Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mzabibu
Yeremia 2 : 21
21 Nami nilikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibumwitu machoni pangu?
Waamuzi 9 : 13
13 Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayumbayumbe juu ya miti?
Isaya 5 : 6
6 nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Yohana 15 : 5
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.
Zaburi 80 : 14
14 Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi, Utazame toka juu uone, uujie mzabibu huu.
Ezekieli 17 : 10
10 Naam, tazama, ingawa umepandwa, je! Utafanikiwa? Hautakauka kabisa, upepo wa mashariki utakapoupiga? Naam, utakauka katika matuta hapo ulipopandwa.
Ezekieli 19 : 14
14 Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.
Leave a Reply