Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mwiba
Mwanzo 3 : 18
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Ayubu 41 : 2
2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
Zaburi 58 : 9
9 ⑥ Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.
Zaburi 118 : 12
12 ⑫ Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
Mhubiri 7 : 6
6 Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili.
Hosea 2 : 6
6 Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake.
Mika 7 : 4
4 Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya walinzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao.
Mathayo 27 : 29
29 Wakasokota taji la miiba, wakaliweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kulia; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!
Marko 15 : 17
17 Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji la miiba, wakamtia kichwani;
Yohana 19 : 2
2 Nao askari wakasokota taji la miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.
Yohana 19 : 5
5 Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa lile taji la miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!
Hesabu 33 : 55
55 ⑬ Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtawabakiza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.
2 Wakorintho 12 : 7
7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
Mithali 22 : 5
5 Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
Mathayo 13 : 7
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
Mathayo 13 : 22
22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Leave a Reply