Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mwanaume
Mwanzo 1 : 27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 2 : 7
7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Mwanzo 5 : 2
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
Kumbukumbu la Torati 4 : 32
32 Tazama siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na kutoka pembe hii ya mbingu hadi ile, kama kumetukia neno lolote kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili?
Ayubu 4 : 17
17 Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?
Ayubu 10 : 3
3 Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Ayubu 10 : 9
9 ⑧ Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
Ayubu 31 : 15
15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?
Ayubu 33 : 4
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
Ayubu 34 : 19
19 ⑱ Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,
Ayubu 35 : 10
10 Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku;
Zaburi 8 : 5
5 Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima;
Zaburi 100 : 3
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
Zaburi 119 : 73
73 ⑯ Mikono yako iliniumba na kunidhibiti, Unifahamishe nikajifunze amri zako.
Zaburi 138 : 8
8 ⑯ BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.
Zaburi 139 : 14
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa njia ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Mhubiri 7 : 29
29 ⑩ Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamepanga mipango mingi.
Isaya 17 : 7
7 Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 42 : 5
5 ⑮ Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
Isaya 43 : 7
7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.
Isaya 45 : 12
12 Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru.
Isaya 64 : 8
8 ⑳ Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
Yeremia 27 : 5
5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio katika nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Zekaria 12 : 1
1 Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Malaki 2 : 10
10 Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?
Marko 10 : 6
6 ⑥ Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwaumba mwanamume na mwanamke.
Waraka kwa Waebrania 2 : 7
7 Umemfanya mdogo kwa muda kuliko malaika, Umemvika taji la utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Leave a Reply