Biblia inasema nini kuhusu mwanamke mzinzi – Mistari yote ya Biblia kuhusu mwanamke mzinzi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mwanamke mzinzi

Mathayo 19 : 9
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Warumi 7 : 2 – 3
2 Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali yule mume akifa, amefunguliwa ile sheria ya mume.
3 Basi wakati mumewe awapo hai, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.

1 Wakorintho 7 : 39
39 Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yuko hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yuko huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu.

Marko 10 : 11
11 ⑧ Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;⑩

Wagalatia 5 : 19
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

Luka 16 : 18
18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

Mathayo 5 : 32
32 ⑳ lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

1 Wakorintho 7 : 10 – 11
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

Kumbukumbu la Torati 24 : 1 – 22
1 ② Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.
3 Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe;
4 ③ yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi.
5 ④ Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yoyote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.
6 ⑤ Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.
7 ⑥ Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwizi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
8 ⑦ Angalia katika pigo la ukoma, utunze kwa bidii, kwa kufanya mfano wa yote watakayowafundisha makuhani Walawi; tunzeni kwa kuyafanya vile vile kama nilivyowaamuru wao.
9 ⑧ Kumbukeni na BWANA, Mungu wako alivyomtenda Miriamu katika njia mlipotoka Misri.
10 ⑩ Umkopeshapo jirani yako chochote kikopeshwacho usiingie katika nyumba yake kwenda kutwaa rehani kwake.
11 Simama nje, yule umkopeshaye akuletee nje ile rehani.
12 Naye akiwa ni mtu maskini, usilale na rehani yake.
13 ⑪ Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za BWANA, Mungu wako.
14 ⑫ Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako;
15 ⑬ mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.
16 ⑭ Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.
17 ⑮ Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;
18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, BWANA, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.
19 ⑯ Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili BWANA, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.
20 Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.
21 Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili; zilizobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.
22 Nawe kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.

1 Wakorintho 7 : 1 – 40
1 Basi kuhusu mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkarudiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
6 Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri.
7 Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.
8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?
17 Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.
18 Je! Mtu fulani ameitwa akiwa amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa akiwa hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.
19 Kutahiriwa si kitu, na kutotahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.
20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa.
21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.
22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.
23 Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu.
24 Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo.
25 Kuhusu wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu.
26 Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo.
27 Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke.
28 Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
29 Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.
31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake ipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.
37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.
38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.
39 Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yuko hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yuko huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu.
40 Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu.

Mithali 7 : 1 – 27
1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.
2 ⑮ Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.
3 ⑯ Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe dada yangu; Mwite ufahamu jamaa yako mwandani.
5 Wapate kukulinda na malaya, Na mwasherati akubembelezaye kwa maneno yake.
6 Maana katika dirisha la nyumba yangu Nilichungulia katika shubaka yake.
7 ⑰ Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
8 Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,
9 ⑱ Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani.
10 ⑲ Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
11 ⑳ Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake.
12 Mara yuko katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia.
13 Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya,
14 Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;
15 Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona.
16 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.
17 Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini.
18 Haya, na tushibe upendo hadi asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.
19 Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali;
20 Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu.
21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.
26 Maana amewaangusha wengi aliowajeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni wengi.
27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *