Biblia inasema nini kuhusu Mwanaharamu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mwanaharamu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mwanaharamu

Kumbukumbu la Torati 23 : 2
2 Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.

Mwanzo 16 : 3
3 Kwa hiyo, baada ya Abramu kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani, Sarai mkewe Abramu alimtwaa Hajiri Mmisri, mjakazi wake, akampa Abramu mumewe, kama mke.

Mwanzo 16 : 15
15 ⑤ Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.

Wagalatia 4 : 22
22 Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Abrahamu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mwingine kwa mwanamke huru.

Mwanzo 19 : 37
37 Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.

Waamuzi 11 : 1
1 Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha.

2 Samweli 11 : 5
5 Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka habari na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja mzito.

Zekaria 9 : 6
6 Na mwana wa haramu atatawala huko Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

Waraka kwa Waebrania 12 : 8
8 ⑱ Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *