Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mwalimu
Mathayo 8 : 19
19 Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.
Mathayo 10 : 25
25 ② Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Mathayo 23 : 8
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
Mathayo 26 : 18
18 ① Akasema, Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.
Mathayo 26 : 25
25 Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.
Mathayo 26 : 49
49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu.
Marko 14 : 45
45 Basi alipokuja, mara akamwendea, akasema, Rabi, akambusu.
Luka 8 : 24
24 Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
Yohana 13 : 14
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha miguu, imewapasa ninyi pia kuoshana miguu ninyi kwa ninyi.
Mathayo 23 : 8
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
Kutoka 21 : 21
21 ③ Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake.
Kutoka 21 : 27
27 Au akimpiga mtumwa wake jino likang’oka, au jino la kijakazi chake, atamwacha huru kwa ajili ya jino lake.
Mambo ya Walawi 19 : 13
13 ⑰ Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ujira wake aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi.
Mambo ya Walawi 25 : 43
43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 5 : 14
14 ⑥ lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
Kumbukumbu la Torati 24 : 15
15 ⑬ mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.
Ayubu 31 : 15
15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?
Mithali 22 : 16
16 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara.
Mithali 29 : 12
12 Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
Mithali 29 : 21
21 Amwendekezaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe.
Yeremia 22 : 13
13 Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;
Malaki 3 : 5
5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
Warumi 4 : 4
4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
Waefeso 6 : 9
9 ⑤ Nanyi, mabwana, watendeeni wao yayo hayo, pasipo kuwatisha, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.
Wakolosai 4 : 1
1 ① Ninyi akina bwana, wapeni watumishi wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Leave a Reply