Biblia inasema nini kuhusu Mvinyo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mvinyo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mvinyo

Mwanzo 40 : 11
11 Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.

Mwanzo 49 : 11
11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.

Isaya 25 : 6
6 ⑲ Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

Yeremia 40 : 10
10 Na mimi, tazama, nitakaa Mizpa, ili nisimame mbele ya Wakaldayo watakaotujia; lakini ninyi chumeni divai, na matunda ya wakati wa jua, na mafuta, mkaviweke vitu hivyo katika vyombo vyenu, mkakae katika miji yenu mliyoitwaa.

Yeremia 40 : 12
12 basi, Wayahudi wote wakarudi kutoka kila mahali walikofukuzwa wakaenda mpaka nchi ya Yuda, wakamwendea Gedalia huko Mizpa, wakakusanya divai, na matunda ya wakati wa jua mengi sana.

Wimbo ulio Bora 8 : 2
2 Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha;[3] Ningekunywesha divai iliyokolea, Divai mpya ya mkomamanga wangu.

Yeremia 13 : 12
12 Basi utawaambia neno hili, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila chupa itajazwa divai; nao watakuambia, Je, sisi hatujui ya kuwa kila chupa itajazwa divai?

Yeremia 48 : 12
12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo nitatuma kwake wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.

Yoshua 9 : 4
4 ⑧ wao wakatenda kwa hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyorarukararuka, na kutiwa viraka;

Yoshua 9 : 13
13 na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa ni vipya; sasa, tazama, vimerarukararuka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana.

Ayubu 32 : 19
19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya liko karibu kupasuka.

Mathayo 9 : 17
17 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.

Luka 5 : 38
38 Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya.

1 Mambo ya Nyakati 27 : 27
27 na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi;

Hagai 1 : 11
11 Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.

Luka 5 : 39
39 Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *