Biblia inasema nini kuhusu Muziki – Mistari yote ya Biblia kuhusu Muziki

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Muziki

1 Mambo ya Nyakati 15 : 22
22 waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi katika uimbaji, asimamie uimbaji, kwa sababu alikuwa stadi.

1 Mambo ya Nyakati 25 : 8
8 ⑧ Wakapigiwa kura ya huduma zao, kwa pamoja, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

2 Mambo ya Nyakati 23 : 13
13 akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao makamanda na wenye parapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga parapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Uhaini! Uhaini!

1 Samweli 16 : 16
16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona.

1 Samweli 16 : 23
23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi alipokishika kinubi na kukipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.

2 Mambo ya Nyakati 29 : 28
28 Na kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, wenye parapanda wakapiga; haya yote yakaendelea hadi ilipomalizika sadaka ya kuteketezwa.

Nehemia 12 : 42
42 na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, akiwa Yezrahia msimamizi wao.

Nehemia 12 : 42
42 na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, akiwa Yezrahia msimamizi wao.

Habakuki 3 : 19
19 MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.[3]

Ezekieli 40 : 44
44 Tena nje ya lango la ndani palikuwa na vyumba kwa waimbaji, katika ua wa ndani, uliokuwa kando ya lango lililoelekea kaskazini, navyo vilikabili upande wa kusini; na kimoja kando ya lango lililoelekea upande wa mashariki, kilikabili upande wa kaskazini.

Ufunuo 5 : 9
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

Ufunuo 14 : 3
3 ⑰ na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale elfu mia moja na arubaini na nne, walionunuliwa katika nchi.

Ufunuo 15 : 3
3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.

Mwanzo 4 : 21
21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba ya wote wapigao kinubi na filimbi.

1 Mambo ya Nyakati 23 : 5
5 na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.

2 Mambo ya Nyakati 7 : 6
6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao walipoagizwa; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.

2 Mambo ya Nyakati 29 : 26
26 ⑫ Wakasimama Walawi wenye vinanda vya Daudi, na makuhani wenye parapanda.

Amosi 6 : 5
5 ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi;

1 Wafalme 10 : 12
12 Mfalme akafanya kwa miti hiyo ya msandali nguzo za nyumba ya BWANA, na za nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haikuja miti ya msandali kama hiyo, wala haikuonekana, hata leo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *