Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mungu
Mwanzo 3 : 21
21 BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Mwanzo 18 : 33
33 Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.
Mwanzo 35 : 7
7 ⑩ Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.
Mwanzo 35 : 9
9 ⑫ Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.
Kutoka 3 : 2
2 ⑤ Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.
Kutoka 19 : 24
24 BWANA akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia BWANA, asije yeye akawafurikia juu yao.
Kutoka 24 : 10
10 ⑱ wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake.
Kumbukumbu la Torati 31 : 15
15 ⑰ BWANA akaonekana katika Hema katika nguzo ya wingu; na ile nguzo ya wingu ikasimama juu ya mlango wa Hema.
Waamuzi 2 : 5
5 Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu;[1] nao wakamchinjia BWANA sadaka huko.
Waamuzi 6 : 24
24 Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu;[8] hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.
1 Wafalme 3 : 5
5 Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.
1 Wafalme 9 : 2
2 ⑮ basi, BWANA akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni.
1 Wafalme 11 : 9
9 ⑦ Basi BWANA akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha BWANA, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,
2 Mambo ya Nyakati 1 : 12
12 basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.
2 Mambo ya Nyakati 7 : 22
22 Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.
Isaya 6 : 5
5 Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.
Ezekieli 1 : 28
28 Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Leave a Reply