Biblia inasema nini kuhusu Muhuri – Mistari yote ya Biblia kuhusu Muhuri

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Muhuri

Mwanzo 38 : 18
18 Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya mhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.

Kutoka 28 : 11
11 Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile mihuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.

Kutoka 28 : 21
21 Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa mihuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hayo makabila kumi na mawili.

Kutoka 28 : 36
36 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa michoro ya mihuri, MTAKATIFU KWA BWANA.

Kutoka 39 : 6
6 ⑧ Nao wakavitengeza vile vito vya shohamu, vilivyotiwa katika vijalizo vya dhahabu, vilivyochorwa mfano wa kuchora kwake mhuri, kwa majina ya hao wana wa Israeli.

Kutoka 39 : 14
14 Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora mihuri, kila moja kwa jina lake, kwa yale makabila kumi na mawili.

Kutoka 39 : 30
30 ⑲ Nao wakafanya hilo bamba la hilo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa mhuri, MTAKATIFU KWA BWANA.

2 Timotheo 2 : 19
19 ① Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.

1 Wafalme 21 : 8
8 Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia mhuri wake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi.

Esta 8 : 8
8 Basi nanyi pia waandikieni Wayahudi vyovyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie mhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa mhuri kwa pete ya mfalme, hakuna awezaye kulitangua.

1 Wafalme 21 : 8
8 Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia mhuri wake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi.

Nehemia 9 : 38
38 Na kwa sababu ya hayo yote sisi tunafanya agano la hakika, na kuliandika; na wakuu wetu, na Walawi wetu, na makuhani wetu, wanalitilia mhuri.

Nehemia 10 : 1
1 Basi hawa ndio waliotia mhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;

Isaya 8 : 16
16 Ufunge huo ushuhuda, ukaitie mhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.

Esta 8 : 8
8 Basi nanyi pia waandikieni Wayahudi vyovyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie mhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa mhuri kwa pete ya mfalme, hakuna awezaye kulitangua.

Danieli 6 : 9
9 Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.

Yeremia 32 : 10
10 Nami nikaitia sahihi ile hati, na kuipiga mhuri, nikawaita mashahidi, nikampimia ile fedha katika mizani.

Kumbukumbu la Torati 32 : 34
34 Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu? Na kutiwa mhuri kati ya hazina yangu?

Danieli 6 : 17
17 Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia mhuri kwa mhuri wake mwenyewe, na kwa mhuri wa wakuu wake, lisibadilike neno lolote katika habari za Danieli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *