Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mto
Zaburi 36 : 8
8 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha kutoka mto wa furaha zako.
Zaburi 46 : 4
4 ⑮ Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
Isaya 32 : 2
2 Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.
Ezekieli 47 : 12
12 Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.
Ufunuo 22 : 2
2 katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Zaburi 119 : 136
136 ⑩ Macho yangu yachuruzika mito ya machozi, Kwa sababu hawaitii sheria yako.
Maombolezo 3 : 48
48 Jicho langu lachuruzika mito ya machozi Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu.
Leave a Reply