Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mtini
Waamuzi 9 : 11
11 Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayumbayumbe juu ya miti?
Yeremia 24 : 3
3 Ndipo BWANA akaniambia, Unaona nini Yeremia? Nikasema, Naona tini; tini nzuri zilizo nzuri sana; na tini mbovu zilizo mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Luka 13 : 9
9 nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.
Luka 21 : 31
31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.
Mathayo 24 : 32
32 Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu;
Ufunuo 6 : 13
13 ⑭ na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
Leave a Reply