Biblia inasema nini kuhusu Mtini – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mtini

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mtini

Hesabu 13 : 23
23 Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu, wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili; wakaleta makomamanga pia, na tini.

Kumbukumbu la Torati 8 : 8
8 nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali;

Zaburi 105 : 33
33 Akaipiga mizabibu yao na mitini yao, Akaivunja miti ya nchi yao.

2 Wafalme 20 : 7
7 Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.

Isaya 38 : 21
21 Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.

Nehemia 13 : 15
15 Siku hizo niliona katika Yuda watu wengine waliosindika zabibu ili kupata mvinyo siku ya sabato, na wengine waliochukua miganda, na kuwapakia punda zao; tena na mvinyo, na zabibu, na tini, na namna zote za mizigo, waliyoileta Yerusalemu, siku ya sabato; nami nikashuhudia juu yao siku ile waliyouza vyakula.

1 Samweli 30 : 12
12 kisha wakampa kipande cha mkate wa tini, na vishada viwili vya zabibu; naye akiisha kula roho yake ikamrudia; kwa maana hakuwa amekula chakula wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.

1 Samweli 25 : 35
35 ⑫ Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimelikubali ombi lako.

Mwanzo 3 : 7
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *