Biblia inasema nini kuhusu Mti wa Palm – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mti wa Palm

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mti wa Palm

Waamuzi 4 : 5
5 Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.

1 Wafalme 6 : 29
29 Akazinakshi kuta zote za nyumba kwa nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, pande za ndani na nje.

1 Wafalme 6 : 32
32 Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende.

1 Wafalme 6 : 35
35 Akanakshi juu yake makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi; akazifunika kwa dhahabu iliyonyoshwa juu ya machoro.

2 Mambo ya Nyakati 3 : 5
5 ⑥ Nayo nyumba kubwa ilizungushiwa miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, juu yake akaichora mitende na minyororo.

Ezekieli 40 : 16
16 Na kwa vile katika vyumba palikuwa na madirisha yaliyofungwa, na kwa miimo yake ndani ya lango pande zote, na kwa matao yake vivyo hivyo; na madirisha yalikuwako, pande zote upande wa ndani, tena palikuwa na mitende juu ya kila mwimo.

Ezekieli 41 : 18
18 kulipambwa kwa makerubi na mitende; mtende mmoja kati ya kerubi na kerubi, na kila kerubi lilikuwa na nyuso mbili;

Yohana 12 : 13
13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!

Kumbukumbu la Torati 34 : 3
3 na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari.

Zaburi 92 : 12
12 Mwenye haki atastawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.

Ufunuo 7 : 9
9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *