Biblia inasema nini kuhusu Mti wa Mkuyu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mti wa Mkuyu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mti wa Mkuyu

1 Wafalme 10 : 27
27 Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifinya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.

2 Mambo ya Nyakati 1 : 15
15 Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.

2 Mambo ya Nyakati 9 : 27
27 ⑮ Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.

Isaya 9 : 10
10 Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake.

1 Mambo ya Nyakati 27 : 28
28 na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;

Zaburi 78 : 47
47 ④ Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe, Na mikuyu yao kwa mawe ya barafu.

Amosi 7 : 14
14 Ndipo Amosi akajibu akamwambia Amazia, Mimi sikuwa nabii, wala sikuwa mwana wa nabii; bali nilikuwa mchungaji, na mtunza mikuyu;

Luka 19 : 4
4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *