Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mtego
Yoshua 23 : 13
13 jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi.
Ayubu 18 : 10
10 Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.
Yeremia 5 : 26
26 Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huvizia kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.
Leave a Reply