Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mpira wa kikapu
2 Timotheo 2 : 5
5 Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria.
Mithali 16 : 3
3 Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli.
Marko 12 : 11
11 Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
2 Petro 1 : 16 – 21
16 Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.
17 Maana alipata heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
18 Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.
19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
21 Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Leave a Reply