Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mpanzi
Mathayo 13 : 8
8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.
Marko 4 : 20
20 Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.
Luka 8 : 8
8 Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikizia, na asikie.
Mhubiri 11 : 4
4 Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
Isaya 28 : 25
25 Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huku na huko kunde, na kutupatupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?
Zaburi 126 : 5
5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
Mithali 11 : 18
18 Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika.
Isaya 32 : 20
20 ⑩ Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng’ombe na punda waende kokote.
Hosea 8 : 7
7 Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.
Hosea 10 : 12
12 Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.
Wagalatia 6 : 8
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Leave a Reply