Biblia inasema nini kuhusu moyo – Mistari yote ya Biblia kuhusu moyo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia moyo

Ezekieli 36 : 26
26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Zaburi 51 : 10
10 ④ Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.

Ezekieli 11 : 19
19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

Yeremia 17 : 10
10 Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.

Mithali 4 : 23
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mathayo 5 : 8
8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Mithali 3 : 5 – 6
5 ③ Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 ④ Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

Yeremia 17 : 9
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Zaburi 34 : 18
18 BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na huwaokoa waliopondeka roho.

Waraka kwa Waebrania 4 : 12
12 ⑳ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Mithali 21 : 2
2 ⑮ Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo.

Warumi 2 : 5
5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,

Zaburi 112 : 7
7 Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumainia BWANA.

Matendo 8 : 22
22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili ikiwezekana, usamehewe fikira hii ya moyo wako.

Yakobo 4 : 8
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Zaburi 26 : 2
2 Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu.

Warumi 1 : 21
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.

Zaburi 97 : 11
11 Nuru humwangazia mwenye haki, Na furaha ni kwa wanyofu wa moyo.

1 Samweli 16 : 7
7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

1 Timotheo 1 : 5
5 Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *