Biblia inasema nini kuhusu Mlima – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mlima

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mlima

Zaburi 97 : 5
5 Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA, Mbele za Bwana wa dunia yote.

Kumbukumbu la Torati 4 : 11
11 ⑫ Mkakaribia, mkasimama chini ya ule mlima; mlima ukawaka moto mpaka kati ya mbinguni, kwa giza na mawingu, na giza kuu.

Kumbukumbu la Torati 5 : 23
23 Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa makabila yenu, na wazee wenu,

Waamuzi 5 : 5
5 ④ Milima ikayeyuka mbele za uso wa BWANA, Naam hata Sinai ule mbele za uso wa BWANA, Mungu wa Israeli.

Isaya 64 : 3
3 Ulipofanya mambo ya kutisha tusiyoyatazamia, ulishuka, milima ikatetemeka mbele zako.

Mika 1 : 4
4 Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.

Nahumu 1 : 5
5 Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.

Ayubu 9 : 5
5 Aiondoaye milima, nayo haina habari, Akiipindua katika hasira zake.

Ayubu 14 : 18
18 Lakini, tazama, mlima ukianguka hutoweka, Nalo jabali huondolewa mahali pake;

Ayubu 28 : 9
9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.

Ezekieli 38 : 20
20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.

Kutoka 3 : 12
12 ⑯ Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.

Kumbukumbu la Torati 12 : 2
2 Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi;

1 Samweli 10 : 5
5 ⑦ Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri;

1 Wafalme 14 : 23
23 Maana hao pia wakajijengea mahali pa juu, na nguzo, na maashera, juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.

Yeremia 3 : 6
6 ⑭ Tena, BWANA akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi.

Hosea 4 : 13
13 ④ Hutoa dhabihu juu ya vilele vya milima, na kufukiza uvumba juu ya vilima, chini ya mialoni na milibua na miela, kwa kuwa uvuli wake ni mwema; kwa sababu hiyo binti zenu huzini, na bibi arusi zenu hufanya uasherati.

Mathayo 4 : 8
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *