Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mlevi
Kumbukumbu la Torati 21 : 21
21 ⑬ Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.
Zaburi 69 : 12
12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
Mithali 23 : 21
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Isaya 28 : 1
1 Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!
Isaya 28 : 3
3 Taji la kiburi la walevi wa Efraimu litakanyagwa kwa miguu;
Yoeli 1 : 5
5 Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
Nahumu 1 : 10
10 Kwa maana kama miiba wametatana, kama walevi wamelewa, watateketezwa kama mabua makavu.
1 Wakorintho 5 : 11
11 ⑤ Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Leave a Reply