Biblia inasema nini kuhusu Mkuki – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mkuki

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mkuki

Ezekieli 39 : 9
9 Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;

1 Samweli 17 : 6
6 Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega yake.

1 Samweli 18 : 11
11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hadi ukutani. Daudi akaepa, mara mbili.

1 Samweli 19 : 10
10 ① Sauli akajaribu kumpiga Daudi hadi ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *