Biblia inasema nini kuhusu Mkono – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mkono

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mkono

Waraka kwa Waebrania 6 : 2
2 na wa mafundisho ya ubatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.

Mwanzo 48 : 14
14 Israeli akanyosha mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.

Kutoka 29 : 10
10 Kisha utamleta huyo ng’ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng’ombe.

Kutoka 29 : 15
15 ③ Pia mtwae kondoo dume mmoja; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo dume.

Kutoka 29 : 19
19 ⑤ Kisha mtwae huyo kondoo wa pili; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo.

Mambo ya Walawi 1 : 4
4 Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.

Mambo ya Walawi 3 : 2
2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 3 : 8
8 Na kuweka mkono wako katika kichwa cha mwana-kondoo yule, atachinjwa mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 3 : 13
13 naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 4 : 15
15 ⑩ Kisha wazee wa mkutano wataweka mikono yao kichwani mwake huyo ng’ombe mbele za BWANA;

Mambo ya Walawi 4 : 24
24 kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.

Mambo ya Walawi 4 : 33
33 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa.

Mambo ya Walawi 16 : 21
21 ⑰ Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, na dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atapelekwa jangwani na mtu aliyetayarishwa kwa ajili ya kazi hiyo[6]

Hesabu 8 : 11
11 naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe watumishi wa BWANA.

Hesabu 27 : 23
23 kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa.

Kumbukumbu la Torati 34 : 9
9 Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama BWANA alivyomwamuru Musa.

1 Timotheo 4 : 14
14 ⑳ Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.

2 Timotheo 1 : 6
6 Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.

Marko 6 : 5
5 ⑪ Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.

Marko 7 : 32
32 Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.

Marko 16 : 18
18 ④ watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.

Luka 4 : 40
40 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.

Matendo 19 : 6
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

Matendo 19 : 11
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *