Biblia inasema nini kuhusu mizizi – Mistari yote ya Biblia kuhusu mizizi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mizizi

Yeremia 17 : 7 – 8
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.

Wakolosai 2 : 6 – 7
6 ⑦ Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, ishini vivyo hivyo katika yeye;
7 ⑧ wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.

Zaburi 1 : 3
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Waefeso 3 : 16 – 19
16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;
18 ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

Waraka kwa Waebrania 12 : 15
15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Marko 4 : 17
17 ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa.

Mathayo 13 : 6
6 Lakini jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *