Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia miungu itafanya
Mithali 3 : 5 โ 6
5 โข Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 โฃ Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
1 Wathesalonike 5 : 16 โ 18
16 Furahini siku zote;
17 ombeni bila kukoma;
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Zaburi 37 : 4
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.
1 Wathesalonike 5 : 18
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Isaya 55 : 8 โ 9
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Waefeso 5 : 17
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
1 Petro 2 : 15
15 โฌ Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;
Yakobo 4 : 13 โ 15
13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;
14 lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.
15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
Zaburi 138 : 8
8 โฏ BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.
Mhubiri 3 : 11
11 โฌ Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Leave a Reply