Biblia inasema nini kuhusu Mispa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mispa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mispa

Yoshua 18 : 26
26 na Mispa, na Kefira, na Moza;

Waamuzi 20 : 3
3 Basi wana wa Benyamini walipata habari ya kuwa wana wa Israeli wamekwea kwenda Mispa. Wana wa Israeli wakasema, Tuambieni huo uovu ulitendekaje?

Waamuzi 20 : 10
10 nasi tutatwaa watu kumi katika mia moja katika kabila zote za Israeli, na watu mia moja katika elfu, na watu elfu katika elfu kumi, ili waende kuwatwalia watu vyakula, ili hapo watakapofika Gibea ya Benyamini wapate kutenda mfano wa upumbavu huo wote walioutenda wao katika Israeli.

1 Samweli 7 : 5
5 ⑮ Samweli akasema, Wakusanyeni Waisraeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA.

1 Samweli 10 : 25
25 Kisha Samweli aliwaambia watu kazi ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za BWANA. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake.

1 Samweli 7 : 16
16 Naye huenda mwaka kwa mwaka kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua katika miji yote ya Israeli.

1 Wafalme 15 : 22
22 ⑰ Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.

2 Mambo ya Nyakati 16 : 6
6 Ndipo mfalme Asa akawatwaa Yuda wote; nao wakayachukua mawe ya Rama, na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye akajenga kwa vitu hivyo Geba na Mispa.

2 Wafalme 25 : 23
23 Kisha, wakuu wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwa mtawala, wakamwendea Gedalia huko Mispa; nao ni hawa, Ishmaeli mwana wa Nethania, na Yohana mwana wa Karea, na Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka, wao na watu wao.

2 Wafalme 25 : 25
25 Lakini ikawa katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, wakampiga hata akafa, na hao Wayahudi na Wakaldayo waliokuwa pamoja naye huko Mispa.

Yeremia 40 : 15
15 Basi, Yohana, mwana wa Karea, akamwambia Gedalia huko Mizpa kwa siri, akisema, Niache niende nikampige Ishmaeli, mwana wa Nethania, wala hapana mtu atakayejua jambo hili; kwa nini akuue wewe, hata wakatawanyike Wayahudi waliokukusanyikia, na mabaki ya Yuda wakaangamie?

Yeremia 41 : 14
14 Basi, watu wote, ambao Ishmaeli amewachukua mateka kutoka Mizpa, wakazunguka, wakarudi, wakamwendea Yohana, mwana wa Karea.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *