Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mipaka ya ardhi iliyoahidiwa
Kutoka 23 : 30 – 31
30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.
31 ⑫ Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.
Ezekieli 37 : 26 – 28
26 ⑳ Tena nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu pangu nitapaweka katikati yao milele.
27 Tena maskani yangu itakuwa pamoja nao; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
28 Na mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, mimi niwatakasaye Israeli, patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao milele.
Hesabu 34 : 1 – 12
1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 ⑭ Waagize wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi ya Kanaani, (hii ndiyo nchi itakayowaangukia kuwa urithi, maana, hiyo nchi ya Kanaani kama mipaka yake ilivyo,)
3 ⑮ ndipo upande wenu wa kusini utakuwa tangu bara ya Sini kupita kando ya Edomu, na mpaka wenu wa kusini utakuwa tangu mwisho wa Bahari ya Chumvi kuelekea mashariki;
4 ⑯ kisha mpaka wenu utageuka kwenda upande wa kusini wa kukwelea kwake Akrabimu, kisha kupita kwendelea Sini; na kutokea kwake kutakuwa kuelekea upande wa kusini wa Kadesh-barnea; kisha utaendelea mpaka Hasar-adari, na kufikia Azmoni;
5 ⑰ kisha mpaka utageuka kutoka Azmoni kwendelea kijito cha Misri, na kutokea kwake kutakuwa hapo baharini.
6 Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; huu ndio mpaka wenu upande wa magharibi.
7 Kisha mpaka wenu wa upande wa kaskazini utakuwa ni huu; kutoka bahari kubwa mtajiandikia mlima wa Hori;
8 ⑱ na kutoka mlima wa Hori mtaweka alama hadi Hamathi; na kutokea kwake mpaka hadi hapo Sedada;
9 ⑲ tena mpaka utatokea hadi Zifroni, na kutokea kwake kutakuwa hapo Hasarenani; huo ndio mpaka wenu wa upande wa kaskazini.
10 Kisha mtaweka mpaka wenu wa upande wa mashariki kutoka Hasarenani hadi Shefamu mpaka Ribla;
11 ⑳ kisha mpaka utateremka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utateremka na kufikia upande wa bahari ya Kinerethi[47] upande wa mashariki;
12 kisha mpaka utateremkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.
Mwanzo 15 : 18 – 21
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.
Leave a Reply