Biblia inasema nini kuhusu mimba – Mistari yote ya Biblia kuhusu mimba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mimba

Yeremia 1 : 5
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua, na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Mwanzo 25 : 21
21 Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

Mwanzo 30 : 22
22 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.

Zaburi 139 : 13 – 16
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa njia ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

Mwanzo 21 : 1
1 BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.

Zaburi 127 : 3 – 5
3 Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.
4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo watoto wa ujanani.
5 Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.

Luka 1 : 37
37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Kutoka 23 : 26
26 ⑦ Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.

Zaburi 113 : 9
9 Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.

1 Samweli 1 : 20
20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume; akamwita Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.

Waamuzi 13 : 3 – 24
3 Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume.
4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
6 Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala hakuniambia jina lake;
7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hadi siku ya kufa kwake.
8 Ndipo huyo Manoa akamwomba BWANA, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa.
9 Mungu akasikia sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye.
10 Basi huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijia siku ile.
11 Basi Manoa akainuka, akamfuata mkewe, na kumfikia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Ndio, ni mimi.
12 Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini?
13 Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, “Hebu huyo mwanamke ajihadhari na yote niliyomwambia.”
14 Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.
15 Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa BWANA, Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako.
16 Lakini malaika wa BWANA akamwambia Manoa, “Ijapokuwa unanizuia, sitakula chakula chako; lakini kama unataka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsogezea BWANA”. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa BWANA.
17 Manoa akamwambia huyo malaika wa BWANA, Jina lako ni nani, ili kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza?
18 Huyo malaika wa BWANA akamwambia, Kwa nini unaniuliza jina langu, na jina hilo ni la ajabu?
19 Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea BWANA hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia.
20 Kwa maana, ikawa, mara huo muali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa BWANA akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakaanguka kifudifudi.
21 Lakini malaika wa BWANA hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa BWANA.
22 Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu tumemuona Mungu.
23 Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
24 Basi yule mwanamke akamzaa mtoto wa kiume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, BWANA akambariki.

Luka 1 : 31 – 35
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume; na jina lake utamwita Yesu.
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye Juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu zake Aliye Juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Kumbukumbu la Torati 7 : 14
14 Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mwanamume wala mwanamke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa kufugwa.

Luka 1 : 36
36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto wa kiume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *