Biblia inasema nini kuhusu Millo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Millo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Millo

Waamuzi 9 : 6
6 Kisha hao watu wote wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika Shekemu.

Waamuzi 9 : 20
20 lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki.

2 Samweli 5 : 9
9 ③ Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.

1 Mambo ya Nyakati 11 : 8
8 Akaujenga huo mji pande zote, toka Milo na kuuzunguka; naye Yoabu akautengeneza mji uliosalia.

1 Wafalme 9 : 15
15 Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hasori, na Megido, na Gezeri.

1 Wafalme 9 : 24
24 Lakini binti Farao akapanda toka mji wa Daudi, mpaka hiyo nyumba yake Sulemani, aliyomjengea; kisha, aliijenga Milo.

1 Wafalme 11 : 27
27 ⑲ Na hii ndiyo sababu ya yeye kumwasi mfalme. Sulemani aliijenga Milo, akapafunga palipobomoka pa mji wa baba yake Daudi.

2 Mambo ya Nyakati 32 : 5
5 ⑪ Hezekia akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.

2 Wafalme 12 : 20
20 Nao watumishi wake wakaondoka, wakala njama, wakamwua Yoashi katika nyumba ya Milo, hapo panaposhukia Sila.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *