Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Milele
Isaya 57 : 15
15 Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Mika 5 : 2
2 ④ Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Zaburi 30 : 12
12 Ili nafsi yangu ikusifu, Wala isinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.
Zaburi 41 : 13
13 Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Amina na Amina.
Zaburi 72 : 17
17 Jina lake na lidumu milele, Pindi ling’aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.
Zaburi 90 : 2
2 ⑩ Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
Zaburi 110 : 4
4 ⑦ BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.
Zaburi 119 : 142
142 ⑬ Haki yako ni haki ya milele, Na sheria yako ni kweli.
Mathayo 6 : 13
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Mathayo 18 : 8
8 Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.
2 Wakorintho 9 : 9
9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.
Leave a Reply