Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Miguu
Isaya 3 : 16
16 BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Isaya 3 : 18
18 Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;
Yohana 13 : 14
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha miguu, imewapasa ninyi pia kuoshana miguu ninyi kwa ninyi.
Kumbukumbu la Torati 33 : 3
3 ⑭ Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako.
Luka 10 : 39
39 Naye alikuwa na dada yake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.
Leave a Reply