Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mieleka
Waefeso 6 : 12
12 ⑧ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Mwanzo 32 : 24
24 ⑮ Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
Mwanzo 30 : 8
8 Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Wafilipi 4 : 13 – 14
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
14 Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.
Waefeso 6 : 12 – 15
12 ⑧ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 ⑩ Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 ⑪ Basi simameni, mkiwa mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 ⑫ na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani;
Mwanzo 32 : 25
25 ⑯ Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
Zaburi 144 : 1
1 ② Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.
Mwanzo 32 : 22 – 32
22 ⑭ Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki.
23 Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo.
24 ⑮ Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 ⑯ Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 ⑰ Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako ni nani? Akasema, Yakobo.
28 ⑱ Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
29 ⑲ Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
30 ⑳ Yakobo akapaita mahali pale, Penieli,[15] maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
31 Jua likamzukia akivuka Penueli, akachechemea kwa sababu ya paja la mguu wake.
32 Kwa hiyo wana wa Israeli hawali ule mshipa ulio katika uvungu wa paja hata leo; maana alimgusa Yakobo panapo uvungu wa paja katika mshipa wa kiuno.
Isaya 41 : 10
10 ② usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
1 Yohana 2 : 15 – 16
15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Leave a Reply