Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia miamba
Zaburi 18 : 2
2 ⑧ BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Zaburi 144 : 1
1 ② Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.
2 Samweli 22 : 32
32 ⑪ Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?
Mathayo 16 : 18
18 ⑯ Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Ufunuo 21 : 11
11 ⑩ ukiwa na utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;
1 Samweli 2 : 2
2 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
Kumbukumbu la Torati 32 : 18
18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.
Leave a Reply