Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mganga
2 Mambo ya Nyakati 16 : 12
12 ① Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali alitafuta msaada wa waganga.
Mathayo 9 : 12
12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa.
Marko 5 : 26
26 na kuvumilia mateso mengi kutoka kwa matabibu wengi, na kugharimiwa mali yake yote aliyokuwa nayo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.
Luka 8 : 43
43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu yeyote,
Marko 2 : 17
17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Luka 4 : 23
23 Akawaambia, Bila shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.
Wakolosai 4 : 14
14 ⑬ Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.
Ayubu 13 : 4
4 Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo, Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.
Yeremia 8 : 22
22 ③ Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?
Luka 5 : 31
31 Yesu akajibu akawaambia, Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio wagonjwa.
Leave a Reply