Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mfuko
Kumbukumbu la Torati 25 : 13
13 Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako.
2 Wafalme 5 : 23
23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamsihi, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakatangulia mbele yake wakiwa wameyabeba.
Mathayo 10 : 10
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mfanyakazi astahili posho yake.
Leave a Reply