Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mfanyakazi Mwalimu
Mithali 8 : 30
30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake;
1 Wakorintho 3 : 10
10 ⑲ Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, niliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
Mwanzo 4 : 22
22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Kutoka 31 : 11
11 na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.
Kutoka 35 : 35
35 ⑪ Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
1 Wafalme 7 : 50
50 na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 14
14 mwana wa mwanamke wa kabila la Dani, na babaye alikuwa mkazi wa Tiro, yeye ni bingwa wa kutumia dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mti; na wa nguo za urujuani, samawati, nyekundu na kitani safi; tena ni stadi kwa kutia nakshi na kuchora michoro yoyote, mbunifu na kuchora chochote kufuatana na kielekezo ambacho angepewa yeye na watu wako mastadi wa bwana wangu Daudi baba yako.
Leave a Reply