Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Meli
Mwanzo 6 : 22
22 ⑥ Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
1 Wafalme 9 : 26
26 Tena, mfalme Sulemani akaunda merikebu huko Ezion-geberi, ulioko karibu na Elothi, pwani ya Bahari ya Shamu, katika nchi ya Edomu.
2 Mambo ya Nyakati 8 : 17
17 ③ Ndipo Sulemani akaenda Esion-geberi, na Elothi, pwani ya nchi ya Edomu.
1 Wafalme 22 : 48
48 Yehoshafati akafanya merikebu za Tarshishi ziende Ofiri kuchukua dhahabu; lakini hazikuenda; kwa maana merikebu zilivunjika huko Esion-geberi.
2 Mambo ya Nyakati 20 : 36
36 ⑭ akapatana naye wakazitengeneza merikebu za kuendea Tarshishi; wakazifanya merikebu zile huko Esion-geberi.
Mwanzo 6 : 14
14 Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje.
Ezekieli 27 : 5
5 Mbao zako zote wamezifanya kwa misonobari itokayo Seniri; wametwaa mierezi ya Lebanoni ili kukufanyia mlingoti;
Isaya 18 : 2
2 Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao.
Mwanzo 6 : 15
15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; dhiraa mia tatu urefu wa safina, dhiraa hamsini upana wake, na dhiraa thelathini kwenda juu.
Yakobo 3 : 4
4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, kokote anakoazimia kwenda nahodha.
Matendo 27 : 40
40 Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo.
Isaya 33 : 23
23 Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.
Matendo 27 : 19
19 Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe.
Isaya 33 : 23
23 Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.
Matendo 27 : 1
1 Basi ilipoamriwa tuabiri hadi Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya ofisa mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.
Matendo 27 : 9
9 Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya,
Matendo 27 : 17
17 Walipokwisha kuikweza wakatumia misaada, wakaikaza merikebu kwa kupitisha kamba chini yake, nao wakiogopa wasije wakakwama katika fungu liitwalo Sirti, wakatua matanga wakachukuliwa vivi hivi.
Matendo 27 : 40
40 Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo.
Ezekieli 27 : 7
7 Tanga lako lilikuwa la kitani safi itokayo Misri, iliyotiwa taraza, ili iwe bendera kwako; na chandarua chako kilikuwa cha rangi ya samawati na urujuani toka visiwa vya Elisha.
Leave a Reply