Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mdaiwa
Kutoka 21 : 6
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.
Kutoka 22 : 15
15 Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama wa kukodisha ni gharama ya kukodisha tu atakayepewa mwenyewe.
Mambo ya Walawi 25 : 17
17 ⑪ Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Mambo ya Walawi 25 : 41
41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake.
Mambo ya Walawi 25 : 55
55 Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Nehemia 10 : 31
31 tena watu wa nchi wakitembeza biashara, au chakula chochote, siku ya sabato, tusinunue kwao siku ya sabato, au siku takatifu; tena mwaka wa saba tusiliwe na madeni yote tuyafute.
Mathayo 5 : 26
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho.
Mathayo 5 : 40
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kulichukua shati lako, mwachie na koti pia.
Mathayo 18 : 25
25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, ikalipwe ile deni.
2 Wafalme 4 : 7
7 Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Nenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
Nehemia 5 : 5
5 Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu.
Ayubu 20 : 19
19 Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang’anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.
Mathayo 18 : 33
33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mtumwa mwenzako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?
Leave a Reply