Biblia inasema nini kuhusu Mbwa mwitu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mbwa mwitu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mbwa mwitu

Mwanzo 49 : 27
27 ③ Benyamini ni mbwamwitu mwenye kuraruararua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.

Yeremia 5 : 6
6 ⑯ Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.

Ezekieli 22 : 27
27 ⑪ Wakuu wake kati yake wamekuwa kama mbwamwitu wakirarua mawindo; ili kumwaga damu, na kuharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.

Sefania 3 : 3
3 Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.

Yohana 10 : 12
12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.

Mathayo 7 : 15
15 ⑳ Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali.

Mathayo 10 : 16
16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

Yohana 10 : 12
12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.

Matendo 20 : 29
29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;

Isaya 11 : 6
6 Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng’ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *