Biblia inasema nini kuhusu Mbwa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mbwa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mbwa

Kumbukumbu la Torati 23 : 18
18 Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.

Ayubu 30 : 1
1 Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao ningewadharau hata kuwasimamia mbwa wa kundi langu.

1 Wafalme 21 : 19
19 Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.

1 Wafalme 22 : 38
38 Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la BWANA alilolinena.

Luka 16 : 21
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa walikuwa wakija na kumramba vidonda vyake.

Mithali 26 : 11
11 Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.

2 Petro 2 : 22
22 ⑦ Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.

Waamuzi 7 : 5
5 Basi akawaleta watu chini majini. BWANA akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa.

Isaya 56 : 11
11 Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.

Mithali 30 : 31
31 Jogoo anayetamba; na beberu; Na mfalme asimamaye mbele ya watu wake.[2]

1 Samweli 17 : 43
43 ⑬ Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.

1 Samweli 24 : 14
14 Na mfalme wa Israeli ametoka ili kumfuatia nani? Unamwinda nani? Ni kuwinda mbwa mfu, au kiroboto.

2 Samweli 3 : 8
8 ⑯ Basi Abneri akakasirika kwa maneno ya Ishboshethi, akasema, Je! Mimi ni kichwa cha mbwa, aliye wa Yuda? Hata leo hivi nawafanyia fadhili nyumba ya Sauli babako, na ndugu zake, na rafiki zake, nisikutie wewe mkononi mwa Daudi; nawe hata hivyo unanitia hatiani leo kwa mwanamke huyu.

2 Samweli 9 : 8
8 ⑮ Akasujudu, akasema, Mimi mtumishi wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi?

2 Samweli 16 : 9
9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake.

2 Wafalme 8 : 13
13 ⑤ Hazaeli akasema, Lakini mimi mtumwa wako ni nani, mimi niliye mbwa tu, hata nifanye jambo hili kubwa? Elisha akajibu, BWANA amenionesha ya kwamba wewe utakuwa mfalme juu ya Shamu.

Isaya 56 : 11
11 Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.

Mathayo 15 : 26
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

Wafilipi 3 : 2
2 ⑬ Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.

Ufunuo 22 : 15
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *