Biblia inasema nini kuhusu mboga – Mistari yote ya Biblia kuhusu mboga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mboga

Mwanzo 1 : 29 – 30
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu;
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

1 Wakorintho 8 : 8
8 Lakini chakula hakitupeleki karibu na Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.

Warumi 14 : 3
3 ⑬ Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.

Mambo ya Walawi 7 : 23 – 24
23 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yoyote, ya ng’ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi.
24 Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa matumizi mengine; lakini msiyale kamwe.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *