Biblia inasema nini kuhusu mbawa – Mistari yote ya Biblia kuhusu mbawa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mbawa

Zaburi 17 : 8
8 ④ Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako;

Ufunuo 12 : 14
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo.

Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Ruthu 2 : 12
12 BWANA akujaze kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.

Isaya 6 : 2
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

Kutoka 25 : 20
20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema.

Zaburi 91 : 4
4 ⑳ Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *