Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mazishi
Warumi 14 : 8
8 ⑯ Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
1 Wathesalonike 4 : 13
13 ⑲ Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
Yohana 11 : 25 – 26
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa, atakuwa anaishi;
26 ⑯ naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Leave a Reply