Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mazimwi
Ufunuo 20 : 1 – 15
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia mhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe kwa muda mfupi.
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa mamlaka ya kutoa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala kuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
5 Hao wafu waliobakia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, kulingana na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 12 : 9
9 Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.
Isaya 27 : 1
1 Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Ufunuo 13 : 1 – 18
1 ① Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, alikuwa na pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya kukufuru.
2 ② Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, lile joka likampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 ③ Nikaona mojawapo wa vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
4 Wakalisujudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
5 ④ Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya kukufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 ⑤ Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
8 ⑥ Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
10 ⑦ Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
11 ⑧ Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili kama Mwana-kondoo, akanena kama joka.
12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
13 ⑩ Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14 ⑪ Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
15 ⑫ Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, ili ile sanamu ya mnyama iongee, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
16 ⑬ Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kulia, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa awe na chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya herufi za jina lake.
18 ⑭ Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Ufunuo 20 : 1 – 3
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia mhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe kwa muda mfupi.
Isaya 51 : 9
9 ⑮ Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Ayubu 40 : 15 – 20
15 Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe; Yeye hula nyasi kama ng’ombe,
16 Tazama basi, nguvu zake zimo katika viuno vyake, Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.
17 Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi; Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18 Mifupa yake ni kama mirija ya shaba; Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.
19 Yeye ni wa kwanza kwa hayo matendo makuu ya Mungu; Ni Muumba wake tu awezaye kumkabili kwa upanga wake.
20 Hakika milima humtolea chakula; Hapo wachezapo wanyama pori wote.
Ufunuo 16 : 13
13 ⑥ Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha lile joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Ayubu 41 : 1 – 34
1 Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3 Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole?
4 Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5 Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6 Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?
8 Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.
9 Tazama, kumtamani ni bure; Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?
10 Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?
11 Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
12 Sitanyamaa kusema habari za via vyake, Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri.
13 Ni nani awezaye kumbambua magamba yake? Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?
14 Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake.
15 Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama yaliyofungwa kwa mhuri.
16 Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati.
17 Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezi kutengwa.
18 Kwa kuchemua kwake mwanga humemetuka, Na macho yake yanafanana na koze za alfajiri.
19 Mienge iwakayo hutoka kinywani mwake, Na cheche za moto huruka nje.
20 Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake, Kama nyungu ikitokota, na manyasi yawakayo.
21 Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake.
22 Katika shingo yake hukaa nguvu, Na utisho hucheza mbele yake.
23 Minofu ya nyama yake hushikamana; Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.
24 Moyo wake una uimara kama jiwe; Naam, uimara kama jiwe la chini la kusagia.
25 Anapojiinua, mashujaa huogopa; Kwa sababu ya woga wao huvunjwa moyo.
26 Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.
27 Yeye huona chuma kuwa kama nyasi, Na shaba kama mti uliooza.
28 Mshale hauwezi kumkimbiza; Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.
29 Marungu huhesabiwa kama mabua; Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.
30 Pande zake za chini ni kama vigae vikali; Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.
31 Yeye hufanya kilindi kichemke kama chungu; Hufanya bahari kuwa kama chungu cha mafuta.
32 Hufanya mapito yake kung’aa nyuma yake Hata mtu angedhani kilindi kina mvi.
33 Juu ya nchi hapana aliyefanana naye, kiumbe asiye na woga.
34 Yeye hutazama kila kitu kilicho juu; Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.
Ufunuo 12 : 1 – 17
1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, akiwa na uchungu na kuumwa katika kuzaa.
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake unakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, limle mtoto wake.
5 Naye akazaa mtoto wa kiume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hadi kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika wake wakapigana na lile joka, lile joka nalo likapigana nao pamoja na malaika wake;
8 lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka lile lilipoona ya kuwa limetupwa katika nchi, lilimfuatia mwanamke yule aliyemzaa mtoto wa kiume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, ili achukuliwe na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule lililoutoa lile joka katika kinywa chake.
17 Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazawa wake waliobakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; nalo likasimama juu ya mchanga wa bahari.
Ezekieli 32 : 2
2 Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Ufunuo 12 : 3 – 4
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake unakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, limle mtoto wake.
Ezekieli 29 : 3
3 nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu.
Zaburi 74 : 13
13 Wewe umeipasua bahari kwa nguvu zako, Umevivunja vichwa vya nyangumi juu ya maji.
Ufunuo 1 : 7
7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na makabila yote ya dunia yataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Ufunuo 12 : 3
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
Ayubu 7 : 12
12 Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi? Hata ukawaweka walinzi juu yangu?
Ufunuo 20 : 2
2 Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
Leave a Reply