Biblia inasema nini kuhusu mayai – Mistari yote ya Biblia kuhusu mayai

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mayai

Isaya 10 : 14
14 Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kiota cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia.

Kumbukumbu la Torati 22 : 6 – 7
6 ⑱ Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wowote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda;
7 ⑲ sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *