Biblia inasema nini kuhusu mawe – Mistari yote ya Biblia kuhusu mawe

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mawe

Mathayo 16 : 18
18 ⑯ Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

Yoshua 4 : 20 – 24
20 Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali.
21 Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini?
22 Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu.
23 Kwa sababu BWANA, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hadi mlipokwisha kuvuka kama BWANA, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka;
24 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, na ili nanyi mpate kumcha BWANA, Mungu wenu, milele.

Ezekieli 28 : 13
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.

Ufunuo 2 : 17
17 ② Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

Danieli 2 : 45
45 ① Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunjavunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.

1 Wafalme 7 : 9
9 Hizi zote zilikuwa za mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, yaliyokatwa kwa misumeno, ndani na nje, tangu msingi hata mawe ya juu, na nje vile vile hata behewa kuu.

2 Mambo ya Nyakati 9 : 9
9 Basi akampa mfalme talanta mia moja na ishirini za dhahabu, na manukato mengi mengi sana, na vito vya thamani; wala hapakuwapo manukato mengi kama hayo aliyopewa mfalme Sulemani na malkia wa Sheba.

Marko 12 : 10
10 Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Yoshua 4 : 2 – 9
2 ⑳ Haya, twaeni watu wanaume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja,
3 kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende na mawe hayo, mkayaweke mahali pale kambini ambapo mtalala usiku huu.
4 Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa ameteua tangu hapo awali, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja;
5 naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya makabila ya wana wa Israeli;
6 ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya?
7 Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yaliondoka mbele ya sanduku la Agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalisimama; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.
8 Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama BWANA alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya makabila ya wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayarundika huko.
9 Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la Agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo.

1 Petro 2 : 5
5 ③ Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *