Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mashtaka, Uongo
Kutoka 23 : 1
1 Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo.
Kutoka 23 : 7
7 Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.
Mambo ya Walawi 19 : 16
16 ⑳ Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu[9] ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
Zaburi 41 : 9
9 Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini, Aliyekula pamoja nami, Ameniinulia kisigino chake.
Mathayo 5 : 11
11 ① Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
Luka 3 : 14
14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
2 Timotheo 3 : 3
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
Mwanzo 39 : 20
20 ⑤ Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani.
Mwanzo 42 : 14
14 Yusufu akawaambia, Ndivyo nilivyowaambia, nikisema, Wapelelezi ninyi.
Hesabu 16 : 3
3 nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yuko kati yao; ya nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?
Hesabu 16 : 13
13 je! Ni jambo dogo, wewe kutuleta kutoka nchi iliyobubujika na maziwa na asali, ili kutuua jangwani, lakini pamoja na haya wajikuza mwenyewe uwe mkuu juu yetu kabisa?
1 Samweli 22 : 16
16 Naye mfalme akasema, Kufa utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya baba yako.
Leave a Reply