Biblia inasema nini kuhusu Mama – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mama

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mama

Kutoka 20 : 12
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 5 : 16
16 ⑦ Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

Mathayo 19 : 19
19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Marko 10 : 19
19 ⑮ Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

Luka 18 : 20
20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.

Waefeso 6 : 2
2 ① Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

Kutoka 21 : 15
15 Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

Kutoka 21 : 17
17 Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

Mambo ya Walawi 18 : 7
7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.

Mambo ya Walawi 19 : 3
3 ⑪ Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 20 : 9
9 Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.

1 Wafalme 19 : 20
20 Naye akawaacha ng’ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Nenda, urudi; ni nini niliyokutendea?

Mithali 1 : 8
8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,

Mithali 6 : 20
20 ⑧ Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.

Mithali 10 : 1
1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

Mithali 15 : 20
20 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye.

Mithali 19 : 26
26 Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye, Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.

Mithali 20 : 20
20 ⑪ Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu.

Mithali 23 : 25
25 Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa.

Mithali 28 : 24
24 Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.

Mithali 29 : 15
15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.

Mithali 30 : 11
11 Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao.

Mithali 30 : 17
17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila.

Mathayo 10 : 37
37 ⑪ Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

Mathayo 15 : 6
6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

Marko 7 : 12
12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *