Biblia inasema nini kuhusu mali za duniani โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu mali za duniani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mali za duniani

Mathayo 6 : 19 โ€“ 21
19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wezi huvunja na kuiba;
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala hawaibi;
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako pia.

Waraka kwa Waebrania 13 : 5
5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.

Mathayo 6 : 24
24 โ‘ข Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Wakolosai 3 : 1 โ€“ 4
1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu.
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.
3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.

Luka 21 : 1 โ€“ 4
1 Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.
2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.
3 Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;
4 maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.

Wafilipi 4 : 19
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Yakobo 4 : 14
14 lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.

Luka 12 : 13 โ€“ 21
13 Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.
14 Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

1 Timotheo 6 : 8
8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.

2 Wakorintho 9 : 7
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.

Mathayo 19 : 23
23 Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Mathayo 6 : 33
33 โ‘ฉ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Wafilipi 4 : 11
11 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *