Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mali
Mwanzo 23 : 18
18 kuwa mali yake Abrahamu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.
Mwanzo 26 : 20
20 ① Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.
Mwanzo 21 : 33
33 Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.
Mwanzo 26 : 22
22 ② Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
Mambo ya Walawi 25 : 30
30 Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika jubilii.
2 Wafalme 8 : 6
6 Na mfalme alipomwuliza yule mwanamke, yeye akamweleza. Basi mfalme akamtolea ofisa, akasema, Mrudishie yote aliyokuwa nayo, na mapato yote ya shamba lake tangu siku aliposafiri, hata leo.
Mambo ya Walawi 25 : 33
33 Tena mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa nyumba iliyouzwa na mji wa milki yake, itatoka katika jubilii; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli.
Mambo ya Walawi 27 : 15
15 Tena mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali yake.
1 Wafalme 21 : 16
16 Ikawa Ahabu aliposikia ya kwamba Nabothi amekufa, akaondoka, aliteremkie shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ili alitamalaki.
Mwanzo 47 : 22
22 ⑪ Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
Hesabu 27 : 11
11 Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Hesabu 36 : 9
9 Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa makabila ya wana wa Israeli yatashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe.
Mhubiri 2 : 21
21 Maana kuna mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na kwa maarifa, na kwa ustadi; naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake. Hayo tena ni ubatili, nayo ni baa kuu.
Kumbukumbu la Torati 19 : 14
14 Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.
Kumbukumbu la Torati 27 : 17
17 ⑩ Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.
Leave a Reply